CLICK HAPA

Saturday, May 12, 2012

OKWI WA SIMBA KAMA MESSI SUDAN

Emmanuel Okwi mchezaji wa Simba, Amekua kivutio kikubwa sana. Kwa mashabiki wa soka nchini Sudan. Kwa habari zilizopati  toka katika benchi la ufundi la timu ya EL AHLY SHANDY  wanahaha jinsi kuwaa walinzi wao mbinu za kumzuia Okwi asiweze kuzifumania nyavu zao.
Mchezo huo ni wamarejeano wa raundi ya 3 ya kombe la shirikisho CAF, na Simba SC wanaitaji sare ya aina yoyote ile ama wasifungwe magoli zaidi ya 2-0 katika mchezo huo.  Simba Sport Club waliichapa El Ahly Shandy goli 3-0 katika mchezo uliochezwa april 29 katika uwanja wa Taifa, na kujiweka katika mazingira mazuri ya kutinga katika hatua ya mwisho ya mtoani, ambapo atapangiwa kucheza na moja ya timu zitakazotolewa katika klabu bingwa Africa. 
Simba waliwasili Sudan mei 9 usiku bila ya beki wake Said Chollo na Juma Saidi Nyosso kufuatia kutakiwa kukosa mchezo huo, kutokana na adhabu za kadi walizopata. Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa mei 10 na Ofisa Habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga ilieleza kuwa wachezaji wa Simba walitelekezwa hotelini kwa zaidi ya saa tano baada ya wenyeji kuwaambia wangewafuata kwa ajili ya safari ya kwenda mji wa Shendi ambako ndiko mechi hiyo itafanyika. Mechi hio itachezwa jumapili 13 May. saa mbili usiku.
 Kikosi hiko baada ya kufika nchini sudan walitekelezwa kwa saa kazaa na baadae waapelekwa kulala mabwenini, chakula wanakipata wa taabu mlo wa mchana wanakula saa kumi jioni. kutokana na hali hio timu ya simba imesema utaifungulia mashitaka timu hio ya sudan kwa shirikisho la soka barani afrika.

HUKUMU YA TAYLOR YAPINGWA

Mawakili wapinga Pendekezo la hukumu ya Taylor
Mawakili wa aliyekuwa Rais wa Liberia Charles Taylor wanasema pendekezo la waendesha mashitaka kuwa ahukumiwe kipindi cha miaka 80 gerezani ni cha kulipiza kisasi. Taylor amepatikana na hatia ya makosa 11 ya kusaidia na kuwafadhili waasi katika vita vya Sierra Leone. Mwendesha mashtaka, Brenda Hollis, wiki iliyopita alisema kifungo hicho kirefu kinaweza kuonyesha jukumu kubwa ambalo Talyor alilitekeleza katika uhalifu wa kiwango kikubwa kama hicho. Mahakama hiyo haina adhabu ya kifo. Katika nyaraka zao zilizowasilishwa kabla ya hukumu kutolewa jumatano wiki ijayo, mawakili wa Taylor wamesema adhabu ya maana inapaswa kuwa idadi fulani ya miaka ambayo inapaswa kuwa chini ya kile kinachoweza kuonekana wazi kama kifungo cha maisha gerezani.

Friday, May 11, 2012

DAWA YA UKIMWI YALETA UTATA

 Jopo hilo limependekeza kwa Mamlaka inayosimamia chakula na Dawa nchini Marekani dawa wakubali dawa aina ya Truvada,itumiwe na watu ambao wamo hatarini kukumbwa na virusi vinavyosambaza ukimwi. Hata hivyo Jopo hilo halina mamlaka juu ya wakuu hao ingawa mara nyingi hukubaliana.
Wahudumu kadhaa wa Afya pamoja na makundi yanayoshughulikia tatizo la ukimwi wamepinga dawa hio isiruhusiwe. Hata hivyo, wandishi wanasema kua hatua hio inaweza kutokea kua muhimu katika vita dhidi ya ukimwi. Tayari dawa ya Truvada imeisha idhinishwa na mamlaka hio ya dawa na chakula kwa watu wanaishi na virusi vya ukimwi, ikitumiwa sambamba na dawa zilizopo maarufu kama ''anti-retroviral drugs''.
Utafiti uliofanywa mnamo mwaka 2010 ulionyesha kua 'Truvada', iliyotengenezwa na kampuni yenye makao yake huko Carlifornia, Gilead Sciences, kwa kiwango ilipunguza hatari ya kuambukizwa ukimwi miongoni mwa wanaume wenye tabia ya kufanya mapenzi na wanaume wenzao kwa asili mia 44% na 73%.Uwamuzi mwezi Juni Kamati inayotoa ushauri kuhusu dawa zinazostahili kutumiwa kwa kukabiliana na ukimwi, FDA, ilipitisha kwa kura 19 kwa 3 kuafiki dawa hii itumiwe na watu ambao wamo katika hatari kubwa kuweza kuambukizwa - wanaume ambao wana tabia ya uzinzi na wanaume wenzao wengi. Vilevile waliidhinisha dawa hii kwa kura nyingi, itumiwe na watu ambao hawajaambukizwa lakini wakiishi na wapenzi ambao tayari wanaishi na virusi vya ukimwi na halikadhalika kwa makundi yanayotazamiwa kua hatarini kuambukizwa ukimwi kupitia shughuli za ngono.


PUTIN HATAHUDHURIA MKUTANO G8


Rais wa Urusi, Vladimir Putin, amemwambia rais Obama kwamba hataweza kuhudhuria mkutano wa mataifa manane yaliyostawi zaidi duniani, maarufu kama G-8, utakaofanyika katika eneo la Camp David nchini Marekani baadaye mwezi huu. Ikulu ya White House imesema kuwa imepata habari kwamba waziri mkuu Dimitry Medvedev atachukuwa nafasi ya rais Putin katika mkutano huo.
Katika taarifa, Washington imesema kuwa bwana Putin hataweza kuhudhuria mkutano huo kwa kuwa anahitaji kukamilisha uteuzi wa baraza lake la mawaziri.Taarifa hiyo imesema kuwa bwana Obama na bwana Putin watafanya mazungumzo katika mkutano wa G20 nchini Mexico mwezi Juni.
                                                     BARACK OBAMA NA PUTIN

SYRIA YATIKISIKA KWA MABOMU


                               MAGARI YALITEKETEA NDANI YAKIWA NA WATU.


MILIPUKO HIO IMEACHA MITARO MIKUBWA KAMA  UNAVYOONA PICHA YA CHINI.
Syria milipuko  miwili  mikubwa  ambayo  imeutikisa  mji  mkuu wa  Syria  Damascus  a, imefanywa  na washambuliaji  wa  kujitoa  muhanga  na  kusababisha  vifo vya   watu  55  na  watu  wengine  372  wamejeruhiwa vibaya. Washambuliaji   waliweka zaidi  ya  kilo 1,000  za  milipuko  katika magari  yao. Hapo kabla  vyombo  vya  habari  vya   taifa  vimesema  kuwa milipuko  hiyo  imewauwa  watu  40  na  kuwajeruhi wengine 200. Mjumbe  wa  kimataifa  kuhusu  Syria  Kofi  Annan ameshutumu vikali   mashambulio  hayo  katika  taarifa iliyotolewa  na  msemaji  wake  Ahmed Fawzi. Annan  amesema kuwa  amesikitishwa  na  upotevu  wa maisha  kutokana  na  mashambulio  hayo  na  anatoa rambi rambi  zake  kwa  familia  za  wahanga.  Annan amesema kuwa vitendo  hivi  vya  kuchukiza  havikubaliki na  ghasia  nchini  Syria  ni  lazima  zikome. Nao  umoja  wa  Ulaya  umeshutumu  vikali mashambulio hayo, na  kuyaeleza  kuwa  ni  vitendo  vya  kigaidi. 

Thursday, May 10, 2012

OBAMA ARUHUSU NDOA ZA MASHOGA MAREKANI



Rais  wa  Marekani  Barack Obama  anaunga  mkono  moja kwa moja ndoa za  watu  wa  jinsia  moja, akiwa  rais  wa kwanza  kufanya  hivyo  nchini  humo.  Obama  amesema kuwa  alisita, kwa sehemu,  kuhusu  ndoa  za  watu  wa jinsia moja  kwasababu  alifikiri  kuwa  mahusiano  ya  watu wawili kwa mujibu wa sheria za kiraia yanatosha. Jana katika  mahojiano  ya  televisheni  katika  ikulu  ya Marekani ameeleza  kuwa alikuwa  na  shaka  kuhusiana na  ukweli  kwamba  watu  wengi  neno  ndoa  ni  jambo ambalo  linazusha  hisia  kali  za  kitamaduni  na  imani  za kidini. Obama amesema  kuwa  kwa  sasa  ni  muhimu  kwake binafsi  kujitokeza  na  kuthibitisha  kuwa   mahusiano  ya watu  wa  jinsia  moja  yanafaa  kufikia  kuwa  watu  hao wanaweza  kuoana.

TIMU YA SIMBA YAINGIA SUDAN KWA KISHINDO LEO


Msafara wa Simba uliondoka jana mchana kwenda Sudan kupitia Nairobi, Kenya tayari kwa mchezo wa marudiano wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Al Ahly Shandy baada ya kukwama kuondoka kutokana na majambazi kuvunja na kuiba katika ubalozi wa Sudan.
Juzi usiku majambazi walivunja sefu ya kuhifadhia fedha na kuiba zaidi ya dola 40,000 ubalozini hapo pamoja fedha nyingine pamoja na kuiba kompyuta zote zinazotumika kuhifadhia kumbukumbu mbalimbali.
Kutokana na hali hiyo, Simba walikwama kupata viza zao. Jana  na saa 10:00 waliondoka kwenda Sudan kupitia Nairobi ikiwa na wachezaji wote wa timu hiyo.
Kwa sasa Simba wameshawasili  Sudan na wanajiweka sawa kwa ajili ya mechi hio ambayo wanahitaji sare ya namna yoyote ili waweze kusonga mbele.




WAZIRI MKUU ATEMBELEA OFISI ZA TUME YA KATIBA MPYA

WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA JANA ALITEMBELEA OFISI ZA TUME YA TAIFA YA KATIBA  NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA TUME HIO KUHUSU CHANGAMAOTO ZINAZOWAKABILI KATIKA ZOEZI HILO LA KUKUSANYA MAONI. NA MWENYEKITI WA TUME HIO AMEWAAMBIA WAANDISHI WAHABARI KWAMBA JENGO HILO LINAMATATIZO YA UMEME KWAHIYO WANAOMBA SERIKALI IFANYA MATENGENEZO KWANI KAZI ZAO ITABIDI ZIFANYIKA PIA USIKU.

MKUTANO WA KUJADILI UCHUMI AFRIKA WAANZA


 Mkutano wa viongozi wa kisiasa na wafanyabiashara wa Kimataifa wameanza mkutano mjini Addis Ababa,Ethiopia kujadili jinsi ya kukuza maendeleo na kuvutia uwekezaji katika bara hilo.

Mkutano huo wa siku tatu juu ya Uchumi Duniani utaangazia masuala kama ajira, utawala bora na kutunza mazingira.

Watayarishi wa mkutano huu wanasema kua Afrika, ni bara lenye nchi sita zenye Uchumi unaokua kwa kasi Duniani na sasa bara hilo liko kwenye ukingo wa mabadiliko makubwa ya uchumi.
Nigeria ni mojapo ya nchi hizo zenye Uchumi unaokua kwa kasi, lakini kama anavyoarifu mwandishi wa BBC Chris Ewokor kutoka Abuja, siyo kila mwananchi aliyenufaika na wimbi hili la mapato.
Ewokor anasema kua majuma matatu yaliyopita Waziri mdogo wa Nigeria katika Wizara ya fedha, Dr Yerima Ngama,alitangaza kua nchi hiyo ni ya tatu kwa nchi zenye Uchumi unaokua kwa haraka.
Alidokezea kua uchumi umeimarika zaidi katika sekta isiyokua ya mafuta, na kwamba serikali ilikua katika jitihada za kuuimarisha zaidi uchumi wake.
Hata hivyo matamshi ya Waziri huyo yanatokea wakati wataalamu wa masuala ya Uchumi nchini Nigeria wakieleza kua nchi hio ina idadi kubwa ya raia wanaoishi maisha duni ya ufukara. Uchumi kwa kiwango kikubwa bado unategemea mafuta. Lakini wa Nigeria wengi ni masikini licha ya utajiri wa mafutla kwa siku

Taarifa ya Benki ya Dunia inasema kua nusu ya watu Afrika wanaishi kwa kipato cha chini ya dola moja kwa kila siku.

Wednesday, May 9, 2012

MAREKANI YASHTUKIA NJAMA ZA MAGAIDI

Maafisa nchini Marekani wanasema kwa ushirikiano na washirika wao kwingineko, wamefanikiwa kutibua njama ya kulipua ndege ya Marekani.
Njama hiyo inadaiwa kuhusisha kilipuzi sawa na kile kilichotumiwa na mshambuliaji aliyejaribu kulipua ndege ya shirika moja la Marekani iliyokuwa ikitoka Yemen kuelekea Marekani mwaka 2009.Maafisa wanasema jaribio hilo lilikuwa limepangwa na kundi moja lenye uhusiani na kundi la al-Qaeda nchini Yemen, na lilipangwa kutekelezwa katika siku ya maadhimisho ya mwaka mmoja tangu kuuawa kwa Osama Bin Laden.
Kilupizi hicho kinafanana na bomu ambayo ilipatikana kwenye chupi ya kijana mmoja raia wa Nigeria aliyefanya jaribo la kulipua ndege mjini Detroit wakati wa mkesha wa krismasi mwaka wa 2009.



BIG BROTHER AFRICA STAR GAME 2012 INATISHA


                                       VICHUPI NJE -NJE KAMA KAWAIDA 
                    MADOVE LOVE KAMA LAST SEASON 
             WASHIRIKI WA BIG BROTHER- MSHIRIKI WA ZIMBWABE DANGER ZONE
                             MSHIRIKI WA TANZANIA YUPO DANGER ZON

On the launch night, 26 housemates entered the house. Big Brother then announced that the first week will be an audition week after which the real housemates will be selected. Big Brother will assign different tasks to the housemates during week 1, the contestants who will do the best will remain as housemates with the chance of winning the grand prize. On day 4, concluding audition week’s tasks, each housemate presented a brief speech about themselves and their country on thursday night task presentation. On day 5, Zeus won the first Amplified head of house task when he picked ball 1 during a task where each housemate picked a ball from a Sputnik in a Game of Chance. In the first friday night Arena games, housemates faced an obstacle course which involved housemates walking on a tight rope in the air which battled with most housemates’ fear of heights. On day 6, Nigeria’s DJ Scratch Master and South African DJ Vigilante graced the first Amplified saturday night live house party with their hiphop mix. On day 7, Namibian musician- Eeez and South African hiphop star- AKA perfomed on the first sunday night live show. During the show the housemates were divided into 2 groups, one with 15 housemates and the other with 11 housemates thereafter living in separate houses-Heads and Tails respectively.

Tuesday, May 8, 2012

MBUNGE NASSARI ANASAKWA NA POLISI ARUSHA


POLISI mkoani hapa imempa Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari (Chadema) saa 12 kujisalimisha vinginevyo adhalilishwe. Polisi pia inashikilia viongozi watatu wa juu wa Chadema, akiwamo Mwenyeki wa Baraza la Vijana la Chadema (Bavita), John Heche, kwa tuhuma za kutoa lugha za uchochezi na ukabila kwa Rais na wananchi wake.  
Habari za kipolisi zinadai kuwa wengine waliokamatwa ni Nelson Mawazo ambaye alikuwa Diwani wa Sombetini (CCM) ambaye hivi karibuni alihama chama hicho pamoja na Mwenyekiti wa zamani wa UVCCM wa Wilaya ya Arusha, Ally Bananga na kujiunga Chadema hivi karibuni. 

Naibu Kamishina wa Jeshi la Polisi nchini, Isaya Mngulu alipoulizwa juu ya hao kukamatwa hakukanusha wala kuthibitisha, bali alisema wanahojiwa kwa maneno waliyotoa kwenye mkutano wa hadhara Jumamosi. ‘’Kweli kuna viongozi wa Chadema tumewakamata baada ya maneno waliyotoa katika mkutano wa hadhara Jumamosi, lakini kwa sasa ni mapema kuyataja,’’ alisema Mngulu.
Hata hivyo, Naibu Kamishina huyo alisema Polisi inamtaka Mbunge huyo ajisalimishe kabla ya saa 12 jioni (juzi) baada ya jitihada za makusudi za kuheshimiana kushindikana ili aende Polisi mwenyewe. Mngulu alisema si kwamba Polisi inashindwa kumpata, bali inampa muda na iwapo utapita bila kujisalimisha, hatua kali za kumsaka zitafanyika na hiyo haitatambua ubunge wake, kwani hayuko juu ya sheria za nchi. ‘’Nassari njoo mwenyewe Polisi vinginevyo itakudhalilisha na haitautambua ubunge wako, kwani wewe hauko juu ya sheria,’’ alisema.

Naibu Kamishina huyo alisema katika mkutano wa hadhara Jumamosi uliohudhuriwa na viongozi kadhaa wa Chadema akiwamo Mwenyekiti Freeman Mbowe,
matamshi ya uchochezi yalitamkwa. Alisema miongoni mwa matamshi hayo ni 

  • ‘’kumpiga marufuku Rais wa Nchi, Jakaya Kikwete, kukanyaga jimbo la Arumeru Mashariki na Kanda ya Ziwa, kwani maeneo hayo ni ya Chadema’’.
  • Mngulu alitaja matamshi mengine ambayo yanamdhalilisha Rais na mwanawe, Ridhiwani, yakihusisha uteuzi anaoufanya Rais kwa viongozi mbalimbali nchini.
Alisema hayo matamshi hayana maana yoyote kwa jamii, kwani yana lengo la uchochezi kwa Rais na wananchi wake. Baada ya matashi hayo jukwaani, Mbowe alisimama na kuyakana akisema si ya Chadema, bali ya vijana hao wenye damu moto wa gesi na ni kauli binafsi na yeye haziungi mkono.

LULU APATA PIGO MAHAKAMANI LEO

Msanii wa filamu za maigizo nchini, Elizabeth Michael ‘Lulu’, leo amepandishwa tena kizimbani mara ya tatu katika kesi ya mauaji ya Kanumba inayomkabili ambapo mawakili wanaomtetea wakiongozwa na Kennedy Fungamtama waliwasilisha ombi la kurekebisha umri wa mshitakiwa huyo kuwa miaka 17 na si 18 kama ilivyowasilishwa mahakamani hapo.
Fungamtama na jopo lake walisema mteja wao ni mtoto mdogo hivyo kesi hiyo ipelekwe mahakama ya watoto na kuwasilisha cheti kinachoonesha ana umri wa miaka 17. Upande wa mashitaka umetupilia mbali ombi hilo na kudai cheti kilichowasilishwa kina mapungufu kadhaa likiwemo jina la Dyana ambalo halijawahi kusikika likitumiwa na mshitakiwa huyo.


         
                           ALIKUA LULU KWELI KWELI MTOTO MASHALAHA
                         LULU AKIINGIA MAHAKAMANI CHINI YA ULINZI MKAL

                          LULU CHINI YA ULINZI MKALI MAHAKAMANI LEO

Monday, May 7, 2012

RAIS AMEWAAPISHA MAWAZIRI LEO IKULU

RAIS WA TANZANIA  MHE. DR JAKAYA MRISHO KIKWETE LEO IKULU AMEWAPISHA MAWAZIRI WOTE ALIOWATEUA BAADA YA BARAZA LA MAWAZIRI WA MWANZO KUJIUZULU KUTOKANA NA KASHFA ZA UFISADI. 
Mawaziri wapya wanaoapishwa na Wizara zao kwenye mabano ni Mbunge wa Handeni,  Dk Abdallah Kigoda (Viwanda na Biashara), Mbunge wa Kalenga, Dk William Mgimwa (Fedha) na Mbunge wa Kuteuliwa, Profesa  Sospeter Muhongo (Nishati na Madini).
Manaibu Mawaziri wapya ni Mbunge wa Rufiji, Dk Seif Suleiman Rashid (Afya na Ustawi wa Jamii), Mbunge wa Kibakwe, George Simbachawene (Nishati na Madini-  Nishati), Mbunge wa Bumbuli, January Makamba (Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia), Mbunge wa Buchosa, Dk Charles Tizeba (Uchukuzi) na Mbunge wa Mvomero, Amos Makala (Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo).
Wengine ni Mbunge wa Makete, Dk Binilith Mahenge (Maji), Mbunge wa Shinyanga Mjini, Stephen Maselle (Nishati na Madini ), Mbunge wa Viti Maalumu, Angela Kairuki (Katiba na Sheria) na wabunge wa kuteuliwa, Janet Mbene na Saada Mkuya Salum ambao wote wamekuwa Manaibu Waziri wa Fedha.

Naibu Mawaziri waliopandishwa na kuwa mawaziri kamili ni Christopher Chiza (Kilimo, Chakula na Ushirika), Dk 
 Harrison Mwakyembe (Uchukuzi), Dk Fenella Mukangala (Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo) na Khamis Kagasheki (Maliasili na Utalii).

Mawaziri wengine waliohamishwa kutoka wizara zao za awali kwenda nyingine ni, Celina Kombani kutoka Katiba na Sheria kwenda Ofisi ya Rais (Manejimenti ya Utumishi wa Umma) ambako amechukua nafasi ya Hawa Ghasia ambaye amehamishiwa Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi).

Shamsi Vuai Nahodha aliyehamia Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa akitokea Mambo ya Ndani, ambako amechukua nafasi ya Dk Hussein Mwinyi ambaye amehamishiwa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.
Dk Emmanuel Nchimbi amehamishiwa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi akitokea Habari, Utamaduni na Michezo wakati Waziri wa Katiba na Sheria sasa ni Mathias Chikawe ambaye alikuwa Ofisi ya Rais (Utawala Bora) na Profesa Jumanne Maghembe amehamishiwa Maji akitokea Kilimo; George Mkuchika ambaye sasa amehamishiwa Ofisi ya Rais – Utawala Bora akitokea Tamisemi na Profesa Mark Mwandosya ambaye ameteuliwa kuwa Waziri katika Ofisi ya Rais, asiyekuwa na Wizara Maalumu. Kabla ya hapo alikuwa Wizara ya Maji.
Manaibu Waziri waliohamishwa wizara zao za zamani zikiwa kwenye mabano ni Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais Charles Kitwanga (Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia), Adam Malima, Kilimo, Chakula na Ushirika (Nishati na Madini) Pereira Ame Silima, Mambo ya Ndani ya Nchi (Fedha).
Wengine ni Gregory Teu, Viwanda na Biashara (Fedha) Lazaro Nyalandu Wizara ya Maliasili na Utalii (Viwanda na Biashara),  Jerryson  Lwenge Ujenzi (Maji).

MATOKEO YA UCHAGUZI UFARANSA

                                                  NICOLAS SARKOZY
Wapiga kura wa Ufaransa wamemchagua  Francois Hollande kutoka chama cha  Socialist kama    rais wao.  Hollande, kwa kiasi kikubwa ajulikani  nje ya mipaka ya Kifaransa, kumpiga nje mfahafidhina Rais Nicolas Sarkozy, ambaye ni mpianaji wa uchumi wa ufaransa ameshindwa kukitetea kiti chake kutokana na sababu mbalimbali     kodi kubwa upiga vita wahamiaji na kupoteza mvuto wa siasa. Rais mpya wa ufaransa ni Francois Hollande.

Sunday, May 6, 2012

SIMBA WAMEIBAKA YANGA 5-0

SIMBA SPORT CLUB BINGWA WA LIGI KUU YA TANZANIA IMESHAICHAPA YANGA BAO 5 KWA 0. GOLI LA KWANZA LILIFUNGWA NA OKWI DAKIKA YA KWANZA NA LA PILI LIMEFUNGWA NA SUNZU......

MASHABIKI WA SIMBA WAKIENDA KUIZIKA YANGA
                    WASHINDI  WA LIGI KUU 2012 SIMBA  WAKIWA WAMEBEBA  

KILIMANJARO THE ROOF OF AFRICA: Mikoa kumi kuwekewa mfumo mawasiliano ya inteneti

KILIMANJARO THE ROOF OF AFRICA: Mikoa kumi kuwekewa mfumo mawasiliano ya inteneti: Mikoa kumi kuwekewa mfumo mawasiliano ya inteneti KAMPUNI ya Six Telecoms Data, imezindua mpango wa kusambaza mfumo mpya wa mawasialino ...

WELCOME TANZANIA THE LAND OF KILIMANJARO & ZANZIBAR

Kilimanjaro is located in northeastern Tanzania and with its tallest peak, Kibo (elevation 19,340 feet [5,895 m]), it is the highest mountain in Africa. Kilimanjaro is roughly 140 miles (225 km) south of Nairobi and roughly 100 miles (160 km) east of the East African Rift Valley. The mountain extends for approximately 50 miles (80 km) east to west and contains three cones - Kibo, Mawensi, and Shira - which are all extinct volcanoes. Kibo is the highest and youngest cone and is linked to Mawensi by a 7 mi (11 km) expanse at roughly 15,000 feet (4,600 m). Mawensi is the oldest cone and is approximately 17,564 feet (5,400 m) high. It is believed that Mawensi was the core of a former summit before Kibo was formed. Shira ridge (elevation 12,395 feet [3,800 m]) is believed to have been a crater in former times

Mikoa kumi kuwekewa mfumo mawasiliano ya inteneti

Mikoa kumi kuwekewa mfumo mawasiliano ya inteneti

KAMPUNI ya Six Telecoms Data, imezindua mpango wa kusambaza mfumo mpya wa mawasialino ya inteneti katika mikoa kumi nchini, ili kupunguza adha ya mawasiliano kwa wakazi wa maeneo ya vijijini. Ofisa Mtendaji Mkuu, Nick Odero, alisema jana jijini Dar es Salaam kuwa, mfumo huo wa mawasiliano unaolikana kama Metro Network, utasambazwa katika mikoa ya Tanzania bara ili kupunguza tatizo la mawasiliano.


"Mfumo huo ni wa kisasa na umekuwa ukitumika katika nchi za bara la Asia na Ulaya, utaunganishwa katika Mikoa ya Dar es Salaam, Arusha, Mwanza, Shinyanga, Kilimanjaro, Dodoma, Morogoro, Iringa, Mbeya na Mtwara," alisema.
Aliongeza,"Metro Network itaondoa tatizo la kukosekana kwa huduma hiyo kwa watumiaji wa mtandao wa mawasiliano ya Inteneti kutokana na kutengenezwa kwa ubora wa hali ya juu."


Alisema kwa watumiaji wa kawaida, huduma hiyo imekuwa ikiwakwaza kutokana na kupata huduma  isiyo bora huku wengine wakiingia gharama kubwa ya kuunganishiwa ili kuweza kutoa huduma bora kwa wateja wao. "Wateja wamekuwa wakipata usumbufu wa hapa na pale na wengine wakishindwa kufanya mawasiliano ya kibiashara na washirika wao. Baada ya kuona usugu wa tatizo hilo, tukaamua kuanzisha huduma hii kwa lengo la kuondoa matatizo hayo,” alisema Odero,"alisema.
Alisema kwa kampuni zilizoko katika majengo marefu ya mikoa kwenye mikoa iliyoingizwa katika huduma hiyo, hawatakuwa na tatizo hilo tena.
Alifafamua kuwa huduma hiyo imetengenzwa kisasa zaidi kupitia utaalamu wa digitali wa ambao tayari kampuni mbalimbai zimeanza kupata huduma hiyo na kuondokana na usumbufu.

border: 0" />

Translate