CLICK HAPA

Saturday, June 23, 2012

KIPANYA KAJA NA MPYA - NANI MDHAIFU?


                    Hiari ya shinda utumwa  - Voluntary is better than force


Kati ya wasanii ambao wanafanya kazi zao kwa weledi basi ni MASOUD KIPANYA ni mmoja wapo.Huyu Jamaa Tangu Mwaka Jana ameamua kuweka background nyeusi(giza) kumaanisha hili ni Taifa la mgao lisilo na suluhisho la kudumu la Nishati ya umeme.Yuko very consistent kwenye fani yake ya uchoraji wa katuni. Atakapojiridhisha kuwa Mgao ni historia(kama ahadi ya JK ilivyo) pengine katuni zake atazichora kwenye plain background. Wahenga walisema Hiari ya Shinda Utumwa
FROM: MDAU

Tuesday, June 19, 2012

MNYIKA ATOA TAMKO NAPE AMLIPUA

MNYIKA ANENA- Nitatoa tamko la kina baadae kuhusu kilichotokea lakini kwa ufupi ubovu wa bajeti hii ni matokeo ya udhaifu wa Rais Kikwete, yeye ndiye aliyesaini Mpango wa Taifa wa miaka mitano kama Kiongozi Mkuu wa Nchi tena kwa wino mwekundu kama Amiri Jeshi Mkuu. Na yeye ndiye Mwenyekitiwa baraza la mawaziri, bajeti hii iliyoacha kuzingatia mpango wa Taifa imepita kwenye baraza alilloliongoza, pia kushindwa kutekelezwa kwa bajeti iliyopita ni matokeo pia ya udhaifu wa taasisi ya Urais. 
  Pia kwa mujibu wa Katiba Rais ndiye ambaye anapeleka bajeti bungeni, Waziri mwenye dhamana anapeleka tu kwa niaba. Rais amepewa mamlakamakubwa juu ya bajeti ibara ya 99 imeweka mipaka kuhusu mambo ambayo bunge lina mamlaka nayo huku ibara ya 90 inasema bunge likikataa bajeti rais ana mamlaka ya kuvunja bunge. Hivyo Rais Kikwete anapaswa kuagiza Waziri wa Fedha bajeti iondolewe irudi kwenye baraza la mawaziri ikafanyiwe marekebisho!




OBAMA NA PUTIN WAKUBALIANA KUHUSU MZOZO WA SYRIA

                                                SYRIA
Rais wa marekani Barack Obama amesema Marekani na Urusi zingependa kuona suluhisho la kisiasa linapatikana nchini Syria na katika kufanikisha hilo watashirikiana na pande nyingine za kimataifa kujaribu kufikia lengo hilo.Viongozi hao wawili wamejikuta kuwa na mwelekeo wa pamoja katika masuala mengi kuhusu Syria wakati wa mazungumzo yao nje ya kikao cha G20 nchini Mexico.Viongozi hao wamejitahidi kuonyesha kuwa mkutano wao uliodumu kwa muda wa saa mbili umeimarisha uhusiano kati yao.

Rais Obama na mwenzake Putin, wamesema kuwa kuna masuala kadhaa kuhusu juhudi za kusitisha maafa nchini syria ambayo wamekubaliana kimsingi.Tumejadiliana kuhusu Syria na tumekubaliana kuwa lazima ghasia zisitishwe na lazima tuwe na mikakati ya kisiasa kuzuia vita vya wenyewe kwa wenyewe na maafa ambayo tumeshuhudia katika kipindi cha hivi karibuni" alisema Rais Obama.

Uhusiano kati ya Marekani na Urusi haujakuwa mzuri sana tangu Rais Putin arudi madarakani mwezi May mwaka huu.Rais Putin hakuhudhuria mkutano wa viongozi wa mataifa tajiri duniani G8 uliofanyika mjini Washingnton nchini Marekani, na wengi walihisi kuwa alisusia mkutano huo. Rais Obama alielezea mkutano wao kuwa wa uwazi na wakina, lakini maneno aliyotatumia yamedhihirisha kuwa pia walitofautiana.

Monday, June 18, 2012

KAZI MBAYA SI MCHEZO MCHAFU

                     
                               A Bad Job Is Not as Worthless As a Good Job
WAHENGA WALISEMA KAZI MBAYA SI MCHEZO MCHAFU. SASA WAGANGA WA JADI WAMEBUNI BIASHARA MPYA BAADA YA KUONA MAISHA YA WATU WENGI WANAITAFUTA TIBA YA  KUJIUNGA NA '''FREEMASON'''     WELCOME BROTHERS......
border: 0" />

Translate