Mzalendo ,mpambanaji na daktari wa binadamu Dr steven ulimboka yu taabani kutokana na mateso aliyosababishiwa na serikali kwa kosa la kudai haki yake na ya madaktari wenzie. sina hakika ni hasira kiasi gani watanzania wengine wanayo kwa kuyashuhudia haya kipindi ambacho wanakabiliwa na magumu ya maisha. tumwombe mungu atupe uvumilivu kama ninaoshindwa kuupata kipindi hiki kigumu.
Siombei yaliyotokea algeria yatokee na tanzania, ila kama mtanzania naiona hatari kubwa ianayoinyemelea taifa letu ya kuweza kuzuka kwa vurugu kutokana na hasira ya wananchi kwa jinsi wanavyoona picha za dr ulimboka aliyeumia vibaya kutokana na kuteswa kupigwa kipindi hiki cha hali ngumu ya maisha nchini.
kwani kumchokoza binadamu yeyote kipindi ambacho anakabiliwa na hali ngumu ya maisha na amekata tamaa humfanya binadamu apoteze uvumilivu na subira na kufanya jambo lolote baya likiwemo Vurugu. Algeria ilikuwa na ugumu wa maisha kwa muda mrefu uliovumiliwa , lakini kitendo cha kujiteketeza kwa moto mohamed bouaziz kutokana na kunyanyaswa na serikali yao kuliwafanya waalgeria wafikie kikomo cha uvumilivu (threshold ), wasiwe na cha kupoteza hivyo kuamua kuingia mitaani bila kuogopa risasi za moto wala mabomu ya machozi, kushinikiza kung"oka rais boteflika hadi kikaeleweka februari 2011.
Mungu ibariki Africa Mungu ibariki Tanzania.
DR ULIMBOKA BAADA YA KUOKOTWA NA AKIPELEKWA HOSPITALI
DR ULIMBOKA ENZI ZAKE ZA UHANAHARAKATI WA KUPIGANIA MASLAHI KWA MADAKTARI- MOJA YA MIKUTANO WAMADAKTARI