CLICK HAPA

Saturday, June 2, 2012

HUNDI YA KWANZA KUTUMIKA

CHECK/CHEQUE AU HUNDI ILIANZA KUTUMIKA 1950 NA BANK YA ENGLAND NDIO BANK YA KWANZA DUNIANI KURUHUSU HUNDI. NA MWAKA 1931 NDIO KULIFANYIKA KONGAMANO LA GENEVA KURUHUSU CHECK/HUNDI KUTUMIKA KIMATAIFA (Geneva convention on the unification of the law relating to cheque)

Friday, June 1, 2012

HUKUMU YA HOSN MUBARAKWA MISRI YAIVA

Rais wa Misri aliyetolewa madarakani mapema mwaka jana Hosn Mubarak, wanawe wakiume wawili na maofisa kadhaa wa usalama wanatarajiwa kujua hatima yao mahakamani Juni 2 mwaka huu.Katika hukumu juu ya tuhuma kadhaa zinazowakabili zikiwamo za rushwa na mauaji ya waandamanaji .Kiongozi huyo, wanawe wawili wakiume na makamanda wa vyombo vya usalama wanatumiwa kwa makosa ya mauaji ya waandamanaji 850 ambao walifariki katika siku18 za mapinduzi yalioung'oa utawala wa kiongozi huyo uliodumu kwa miongo mitatu.
Katika tuhuma za rushwa zinazomkabili Mubarak , ni kuuzwa kwa benki ya Al-Watany ambapo yeye na familia yake walinunua hisa zote ambazo zlipaswaa kununuliwa na watu wa kawaida. Sambamba na hilo walichota Euro milioni 300 na kuzificha katika mabenki za ng'ambo.

Aliyekuwa Rais wa Misri Hosn Mubarak akiwa mahakamani
Kulingana na taarifa zilizotolewa na Televisheni ya Nile, Gamal Mubarak mtoto wa Mubarak aliyekuwa katika kamati maalumu ya Chama kilichokuwa kinatawala wakati huo na aliyetazamwa kama mrithi wa baba yake alitoa maamuzi mengi. Huku mtoto mkubwa wa kiongozi huyo Alaa aliyekuwa kando ya ulingo wa siasa akituhumiwa kwa kujihusisha mno na utesaji wa watu kadhaa, wakati wa utawala wa baba yake.Watoto hawa wakiwa rumande katika gereza moja jijini Cairo wanasubiri hukumu yao jumamosi hii sambamba na baba yao mwenye umri wa miaka 84 anayezuiliwa katika hospitali moja ya kijeshi anakotibiwa ugonjwa wa moyo.

Wednesday, May 30, 2012

CHARLES TAYLOR AHUKUMIWA MIAKA 50 JELA.



Charles Tayler aliyekua rais wa Liberia amehukumiwa na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu kwa ajili ya Sierra Leone leo imetoa adhabu ya kifungo cha miaka 50 jela kwa dikteta wa zamani wa Liberia, Charles Talyor. Akisoma hukumu hiyo muda mchache uliopita, Jaji Richard Lussick amesema kwamba jopo la majaji limeamua kwamba Taylor atatumia kifungo chake kwa awamu moja. Mahakama hiyo ilimtia hatiani Taylor mwenye umri wa miaka 64, hapo mwezi Aprili. Taylor alipatikana na makosa ya kuwafadhili na kuwapa silaha waasi wa United Revolution Front (URF) wa nchi jirani ya Sierra Leone  wakati nchi hiyo ikiwa kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe. Katika vita hivyo vya baina ya mwaka 1992 na 2002, kiasi ya watu 120,000 waliuawa. Wakili wa upande wa mashtaka amemPa kifungo cha miaka 80 dhidi ya Taylor. Kesi yake iliyoanza mwaka 2007 ilishuhudia watu kadhaa maarufu wakihusika, akiwamo mwanamitindo wa Kimarekani, Naomi Campbell, ambaye alisimama kizimbani kama shahidi. Kesi hiyo ilihamishiwa kutoka Afrika ya Magharibi na kufanyika nchini Uholanzi kwa sababu za kiusalama 

                                Charles Taylor akiwa The Hague mahakamani

Tuesday, May 29, 2012

MATUKIO YA UZINDUZI WA TAWI LA CHADEMA WASHINGTON MAREKANI

CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO CHADEMA TAREHE 27 MAY 2012 KILIFUNGUA TAWI LA WASHINGTON DC. TAWI HILO LILIFUNGULIWA MHE ZITTO KABWE NAIBU KATIBU MKUU WA CHADEMA  AKIWA AMEAMBATANA NA VIONGOZI MBALIMBALI WA CHAMA HICHO MCHUNGAJI PETER  MSIGWA, JOSHUA NASSARI, NA L.NYERERE NA MSABAHA WOTE NI WABUNGE WA BUNGE LA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA.

Zitto Kabwe alisema lengo la matawi hayo ni kupata fikra na mawazo yatakayoisaidia nchi na sio sehemu ya kufanya majungu ya kudanganya viongozi wakuu wa nchi wanaokwenda nchini humo.“Matawi ya Chadema Washington DC sio kama ya CCM ambayo yakikaa yanawaza rais au waziri mkuu akija wamdanganye nini, wapeleke umbea gani au ‘kuchomana’ Watanzania wenyewe kwa wenyewe…hatutaki hayo; tunataka yawe kisima cha fikra na mawazo ya kuiendeleza nchi,” alisema.

Katika uzinduzi huo, Watanzania kadhaa waishio Marekani walichukua kadi za Chadema.

                                            ZITTO AKIFUNGUA MKUTANO HUO
                                         TIMU YA CHADEMA ILIYOWENDA MAREKANI
              WATANZANIA WAISHIO MAREANI WALIOJIUNGA NA CHADEMA
                                         WALIOJIUNGA NA CHADEMA
      ZITTO NAIBU KATIBU CDM AKIWA NA MWENYEKITI WA CHADEMA WASHINGTON            NDUGU KALLEY PANDUKIZI
                             WANACHAMA WAPYA KUTOKA WASHINGTON
       

     PIA WALITEMBELEA UBALOZI WATANZANIA MAREKANI NAKUPOELEWA NA BALOZI        WA TANZANIA NCHINI MAREKANI MHE. MWANAIDI SINARE MAAJA

Monday, May 28, 2012

ZANZIBAR YACHAFUKA MABOMU SIKU NZIMA

Hali isiyokua ya kawaida imevikumba visiwa vya Zanzibar, kanisa  la choma moto watu zaidi ya 46 wakamatwa na jeshi la polisi visiwani huko na mabomu ya machozi yapigwa siku nzima madua yafungwa watu wajifungia ndani. Hali hii imesababishwa  na kuandamana pasipo na kibali. Waandamaji hao waliokua  na madai mawili makuu kwa serikali ya mapinduzi Zanzibar kutaka viongozi wao waliokamatwa wakidai Zanzibar ijitenge na Tanzania bara waachiwe huru bila hivyo watavamia kituo cha polisi kinachowashikilia  na dai la pili ni serikali ya visiwa hivyo kuitisha kura ya maoni kama serikali muungano wa jamuhuri ya Tanzania uendelea au usiendelee. Wanaharakati hao ni wafuasi wa kikundi kimoja cha kidini chenye msimamo mkali katika visiwani vya  Zanzibar.
                BARABARA ZILIFUNGWA NA KUCHOMA MATAIRI
                                                       WAANDAMANAJI




                                           VIONGOZI WA MAANDAMANO HAYO
KANISA LILILOCHOMWA MOTO

Sunday, May 27, 2012

SIMBA NDANI YA DAR LIVE KUSHEREKEA UBINGWA.

SIMBA NDANI YA DAR LIVE KUSHEREKEA USHINDI HUKU WA KIMUENZI MAFISANGO. MASHABIKI NA WAPENZI WA TIMU YA SIMBA SPORT CLUB MNAKARIBISHWA.




border: 0" />

Translate