Rais wa Misri aliyetolewa madarakani mapema mwaka jana Hosn Mubarak, wanawe wakiume wawili na maofisa kadhaa wa usalama wanatarajiwa kujua hatima yao mahakamani Juni 2 mwaka huu.Katika hukumu juu ya tuhuma kadhaa zinazowakabili zikiwamo za rushwa na mauaji ya waandamanaji .Kiongozi huyo, wanawe wawili wakiume na makamanda wa vyombo vya usalama wanatumiwa kwa makosa ya mauaji ya waandamanaji 850 ambao walifariki katika siku18 za mapinduzi yalioung'oa utawala wa kiongozi huyo uliodumu kwa miongo mitatu.
Katika tuhuma za rushwa zinazomkabili Mubarak , ni kuuzwa kwa benki ya Al-Watany ambapo yeye na familia yake walinunua hisa zote ambazo zlipaswaa kununuliwa na watu wa kawaida. Sambamba na hilo walichota Euro milioni 300 na kuzificha katika mabenki za ng'ambo.
Aliyekuwa Rais wa Misri Hosn Mubarak akiwa mahakamani
Kulingana na taarifa zilizotolewa na Televisheni ya Nile, Gamal Mubarak mtoto wa Mubarak aliyekuwa katika kamati maalumu ya Chama kilichokuwa kinatawala wakati huo na aliyetazamwa kama mrithi wa baba yake alitoa maamuzi mengi. Huku mtoto mkubwa wa kiongozi huyo Alaa aliyekuwa kando ya ulingo wa siasa akituhumiwa kwa kujihusisha mno na utesaji wa watu kadhaa, wakati wa utawala wa baba yake.Watoto hawa wakiwa rumande katika gereza moja jijini Cairo wanasubiri hukumu yao jumamosi hii sambamba na baba yao mwenye umri wa miaka 84 anayezuiliwa katika hospitali moja ya kijeshi anakotibiwa ugonjwa wa moyo.
No comments:
Post a Comment