CLICK HAPA

Wednesday, September 12, 2012

UBALOZI WA MAREKANI LIBYA WATEKETEA

Balozi wa Marekani nchini Libya ameuawa baada ya kushambuliwa na watu waliokuwa wamejihami na kuvamia ubalozi wa Marekani Mashariki mwa mji wa Benghazi. Balozi J Christopher Stevens, ni miongoni mwa maafisa wengine wa ubalozi waliouawa kufuatia maandamano kuhusu filamu iliyotolewa nchini humo ikimkejeli Mtume MuhammadIdara ya mambo ya ndani nchini Marekani, imethibitisha tu kifo cha afisaa mmoja wa ubalozi huo ingawa bado haijataja jina lake
Maandamano ya kupinga filamu hiyo pia yalifanyika mjini Cairo dhidi ya ubalozi wa Marekani.Wakati huohuo, waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bi. Hilary Clinton, amelaani mashambulizi hayo.
Serikali ya Libya imetaja shambulio hilo kama kitendo cha uoga.
Ubalozi huo uliteketezwa na watu waliojihami kwa bunduki kulalamikia filamu moja iliyotengenezewa nchini Marekani ambayo wanasema inamdhihaki Mtume Mohammed. Wanamgambo hao wanaoripotiwa kuwa na ufungamano na kundi la waislamu wenye msimamo mkali walitumia maguruneti ya kurushwa kwa roketi kuvamia ubalozi huo kabla ya kuiteketeza. Maafisa wa Libya wameiambia BBC kwamba hali imetulia kwa sasa.
Machafuko hayo ya Libya yalijiri saa kadhaa baada ya maelfu ya waandamanaji kukusanyika nje ya ubalozi wa Marekani mjini Cairo kuelezea hasira zao kuhusu filamu hiyo kumhusu Mtume Mohammed.
Kwa wakati mmoja waandamanaji hao waliingia ndani ya ubalozi huo na kuichana bendera ya Marekani na kurejesha yao.
                         WAANDAMANAJI WAKICHANA BENDERA YA MAREKANI

   BALOZI WA MAREKANI ALIYEPOTEZA MAISHA KATIKA SHAMBULIZI HILO

Tuesday, September 11, 2012

WAANDISHI WA HABARI KILIMANJARO WAMLILIA DAUDI MWANGOSHI

   WAANDISHI WA HABARI MKOA KILIMANJARO NAO WALIUNGANA NA WAANDISHI WENZAO TANZANIA KUITIKIA WITO WA CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI TANZANIA   WA KUPINGA MAUAJI YALIYOFANYA NA JESHI LAPOLISI KWA KUMUUA MWANDISHI MWENZAO DAUDI MWANGOSI WA CHANNEL TEN ALIYEPIGWA BOMU NA POLISI MKOANI IRINGA


PIA WALIBEBA MABANGO MBALIMBALI YAKIPELEKA UJUMBE KWA JESHI LA POLISI


MAANDAMANO HAYA YAMEFANYIKA KITAIFA MKOANI DAR ES SAALAM NA WAZIRI WA MAMBO YA NDANI MHE. NCHIMBI  ALIUDHURIA BILA MWALIKO. NIA YA MHE. NCHIMBI NI  KUPOKEE  MAANDAMANO HAYO LAKINI  ALIFUKUZWA NA WAANDISHI WA HABARI NA KUSEMA WALIKUWA HAWAJAMWALIKA

border: 0" />

Translate