CLICK HAPA

Saturday, June 9, 2012

MATUKIO YA JANGWANI- CCM INAWENYEWE

Mkutano umemalizika kwa amani lakini kwa ujumla katika wazungumzaji wote wa CCM na mawaziri walioongea aliyeonekana kuwagusa watu wengi ni Waziri wa uchukuzi Dr Harisson Mwakyembe na magufuli ambaye alitoa hadi namba yake ya simu 0782242526 kumpigia wakati wowote mwananchi atakapokumbana na adha yoyote kwenye sekta ya usafiri.  pili magufli leo ametoa mpya aongea ziadi ya lugha10 za makabila ya Tanzania. 
VIONGOZI WA CCM WALIOUDHURIA

                  KADI ZA VYAMA PINZANI ZILIZORUDISHWA NA KUJIUNGA NA CCM
 WAZIRI WA MIUNDO MBINU HARRISSON MAKYEMBE AKIMWAGA SERA ZA CCM              ZINAZOTEKELEZWA NA WIZARA YAKE
WANACHAMA NA WAPENZI WA CHAMA TAWALA DAR ES SALAAM WALIJITOKEZA KWA WINGI KATIKA VIWANJA VYA JANGWANI

NAPE- ANASEMA KARIBUNI JANGWANI



 Maudhui;  “ Kutoa Msimamo Wake Juu ya Masuala Yanayogusa Mustakabali wa Taifa. Hivyo Chama Kitatumia Fursa hiyo Kuelezea Watanzania Juu ya Msimamo Wake Katika Mambo yafuatayo:
1.     Hatma ya maisha ya Watanzania
·        Ajira
·        Miundo mbinu ya Barabara, Reli, Bandari Na Anga.
·        Bei za bidhaa mbalimbali.
·        Umeme
·        Rasilimali za taifa
2.     Msimamo wa Chama Cha Mapinduzi kuhusu Mchakato wa Katiba Mpya.
3.     Vurugu za Zanzibar.
LEO SAA 8 MCHANA VIWANJA VYA JANGWANI

Friday, June 8, 2012

CCM KESHO NDANI YA VIWANJA VYA JANGWANI

TANGAZO:

Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kimeandaa Mkutano Mkubwa wa Hadhara kwa wananchi wote, Siku ya Jumamosi, tarehe 09/06/2012, Katika Viwanja vya Jangwani Kuanzia saa 8 mchana. 
  Maudhui;  “ Kutoa Msimamo Wake Juu ya Masuala Yanayogusa Mustakabali wa Taifa. Hivyo Chama Kitatumia Fursa hiyo Kuelezea Watanzania Juu ya Msimamo Wake Katika Mambo yafuatayo:

1.     Hatma ya maisha ya Watanzania
·        Ajira
·        Miundo mbinu ya Barabara, Reli, Bandari Na Anga.
·        Bei za bidhaa mbalimbali.
·        Umeme
·        Rasilimali za taifa

2.     Msimamo wa Chama Cha Mapinduzi kuhusu Mchakato wa Katiba Mpya.

3.     Vurugu za Zanzibar.


Katika Mkutano huo, Viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali watakuwepo na kutoa ufafanuzi juu ya masuala hayo yaliyoainishwa kama msimamo wa Chama Cha Mapinduzi.

Chama Cha Mapinduzi, kinawaalika wanachama wake wote, wakereketwa na wananchi kwa ujumla kuhudhuria katika mkutano huo mkubwa. Mkutano utafanyika kwa amani na utulivu na wote mnakaribishwa.

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
Imetolewa na:

JUMA SIMBA
KATIBU WA SIASA NA UENEZI
MKOA WA DAR ES SALAAM.
07/06/2012

Thursday, June 7, 2012

TAWI LA CHADEMA WASHINGTON DC LAZIDI KUKUA

Mwenyeketi wa  Tawi la Chama Cha Demokrasia CHADEMA Washington DC Kalley Pandukizi akiwa na katibu wachama hicho,Ndugu Libe Mwang'ombe alipotoa kadi rasmi kwa Beautician maharufu na designer wa kiTanzan Linda  Bezuidenhout (LB)

Katika miaka ya nyumba Linda aliwahi  kusponsor  matukio mbali mbali kwenye  miaka ya 1990 wengi wao wakimjua kwa Linda Express Nchini Tanzania ambae ambaye hivisasa anajishughulisha na  biashara ya nguo za kiume milanovita.com pamoja na  zakike ambazo anadesign mwenyewe kwa brand name ya Linda kutoka Atlanta, Georgia Nchini Marekani
Mwenyeketi wa tawi la Tawi la Chama Cha Demokrasia CHADEMA Washington DC Mhe.  Kalley pamoja na katibu wake  Mhe. Libe Mwang'ombe wakipata picha ya pamoja na Linda  Bezuidenhout Atlanta, Georgia na wanachama wa tawi la chadema Washington DC
Mwenyeketi wa tawi la Tawi la Chama Cha Demokrasia CHADEMA Washington DC Mhe. Kalley Pandukizi, pamoja na katibu wake  Mhe. Libe Mwang'ombe akimkabidhi rasmi mwanacham mkareketwa  ambae ni mwana mitindo Linda  Bezuidenhout (LB) kati ya uwanachama wa chama cha  Demokrasia Chadema katika ofisi ya  tawi la Tawi la Chama Washington DC.




Linda Bezuidenhout (LB) furaha baada ya kuvua gamba kuvaa gwanda na kuchukua kadi  kuwa mwanachama kamili wa Chama Cha Demokrasia Chadema.

MBUNGE WA ROMBO ATOA SHUKRANI


Monday, June 4, 2012

NAPE APATA MAPOKEZI YA KIFALME SONGEA

KATIBU WA HALAMASHAHURI KUU CCM NAPE  AUTEKA MJI WA SONGEA BAADA YA KUPOELEWA KWA UMATI AMBAO HAUJAPATA TOKEA KATIKA MJI SONGEA. NAPE YUPO KIZIARA  SONGEA KWA AJILI YA KUFUNGUA JENGO LA MABANDA 119  KWA WAFANYABISHARA NDOGONDOGO NA KUBWA.  JENGO HILO LINAMILIKIWA NA CCM LENYE THAMANI YA SHILINGI MILLION 206. PIA HATAFANYA MIKUTANO YA KUIMARISHA CHAMA.
                    WANAWAKE WA MJI WA SONGEA WAKIMKARIBISHA NAPE
                                       NAPE AKIPITA JUU YA KANGA






Sunday, June 3, 2012

SIKU YA MAZINGIRA DUNIANI - MOSHI

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipanda mti aina ya Mroliondo katika eneo la Chem chem ya Maji Njoro,leo Juni 03, 2012, ikiwa ni sehemu ya uzinduzi wa Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani yanayofanyika Kitaifa Mkoani Kilimanjaro.

Kwa muda mrefu sasa, Makamu wa Rais amekuwa mwanamazingira aliye mstari wa mbele katika usimamizi na uboreshaji wa mazingira na hali ya hewa kwa ujumla. Amekuwa akishiriki katika ziara mbalimbali za kimazingira na hali ya hewa ndani na nje ya nchi.

border: 0" />

Translate