CLICK HAPA

Saturday, May 19, 2012

MTANZANIA WA KWANZA KUPANDA MLIMA EVEREST

      Leo 19-5-2012  asubuhi  mtanzania Wilfred Moshi amefanikiwa kupanda mlima mrefu kuliko yote duniani. Mlima Everest upo ulaya una urefu wa mita 8845 au (29029futi) ni mkubwa zaidi ya mlima Kilimanjaro wenye urefu mita 5895. 
      Katika historia mtu wa kwanza upanda mlima Evarest walikuwa waingereza wawili Tenzing na Hillary mwaka 1953 na mwanamke wa kwanza upanda mlima everest ni mjapani anaitwa Junko Tabei mwaka 1975. Waliofanikiwa kupanda mlima huo kwa mara ya kwanza bila kutumia vifaa vya oksijeni ni  Reinhod Messer (Italy) na Peter Habeler (Austria) mwaka 1980. Aliyefanikiwa kupanda mlima huo kipindi cha baridi kali ni raia wa Poland Andrzej Zawada. Mwaka 1996 wapandaji 16 walikufa katika mlima huo. Na mtu anayeshikilia rekodi ya kupanda mlima huo mara nyingi kuliko wote ni Apa Sherpa amepanda mara 21, na aliyepanda mlima huo akiwa na umri mkubwa zaidi ni Min Bahadur Sherchan.
  Gharama za kupanda mlima huo ni kubwa sana ni dola 15000 za marekani ikiwa ni gharama za kupanda, Bado gharama za matiba, chakula  na wasaidizi na usafiri zinakaribia 40000/80000 dola za kimarekani inategemea na njia utakayotumia kupandia.
  Pamoja na gharama zote hizo Mtanzania Wilfred Moshi aliweka dhamira ya upanda mlima huo, Alipokua anaondoka alisema nimenunua hii bendera ya Tanzania na gharama zinazofanikisha safari yangu nimechangiwa lakini sio na Watanzania. Watanzania mnachoweza kufanya sasa ni kuniombea kwa Mungu.

       WiILFRED MOSHI AKIWA NA BENDERA YA TANZANIA JUU YA MLIMA EVEREST
        HAPA NDIPO SAFARI YA KUPANDA ILIPOANZIA AKIWA NA TIMU YA WASAIDIZI

KILELE CHA MLIMA EVEREST CHENYE MITA 8845
                               WILFRED MOSHI KOTI JEKUNDU- SI KAZI RAHISI KUPANDA

3 comments:

  1. WELL DONE WILFRD,
    Nakupongeza kwwani umetimiliza dhamira yako toka awali ukiandaa inurance cover ya kusafiri niliiishughulikia katika kampuni yetu ya phoenix of Tanzani8a assurance co.ltd.kupitia tawi letu la arusha.Mungu amaefanya kile ulichokusudia na tunakuombea urejee nyumbani salama.

    ReplyDelete
  2. TUNAPASWA KUJIVUNIA HUYU NDUGU

    ReplyDelete
  3. Watanzania tunaweza kujivunia tukiwa na nia tunaweza kufanya kufanya kitu tuige mfano wa Wilfred. sababu tunayo na uwezo tunao

    ReplyDelete

border: 0" />

Translate