CLICK HAPA

Saturday, May 26, 2012

NAPE NNAUYE ANENA CCM HAITAKUFA

Katibu wa halmashauri kuu ya CCM (NEC) Nape Nnauye Itiadi na Uenezi amesema CCM Haitakufa hata akibaki yeye mwenyewe. Pia amewahasa vijana kupenda kuchukia rushwa kwa watu wenye fedha wanaotoka mijini na kuwaachia madaraka bila wao kujua hatima yao kwani watakufa bila kujiongoza, Pia amesema CCM wataondoa utaratibu wa watu kutoka mijini na kuja vijijini kipindi kwa uchaguzi na kupewa ridhaa ya chama kugombania nafasi mbalimbali. Nape aliyasema hayo alipokua Missenyi kwenye  Baraza la Vijana.
                NAPE AKIPOKELEWA NA GWARIDE MISSENYI- BARAZA LA VIJANA
   

MISS MOSHI ASAKWA USIKU WALEO

MLIMBWENDE WA MOSHI ASAKWA USIKU WA LEO. WADHAMINI WA SHUNGHULI HIO YA KUMTAFUTA MALKIA WA MJI HUO NI  NI PANONE & CO. LTD, SPARD LTD, MORGAN SOUND.

AL-SHABAAB WASAMBARATISHA

Vikosi vya muungano wa nchi za Afrika vimefanikiwa kuuteka mji muhimu karibu na  Jiji Mogadishu. Mji huo wa Afoye  ulikua unatumia na kundi hilo kushambulia jiji la mogadishi na uhunganisha jiji hilo magharibi na kusini kwani lina njia muhimu kuingia jiji la Mogadishu. Vikosi vya AU vimeuzingira mji huo na vifaru na wapiganaji wa Al-Shabaab inasadikiwa wamejificha katika vichaka na mashamba. Kwa kupoteza eneo hilo ni pigo kubwa kwa kundi hilo ni sehemu muhimu.

                                       VIKOSI VYA AL - SHABAAAB

Friday, May 25, 2012

MAAJABU YA MATUNDA NI TIBA ILIYODHARAULIWA

Karoti ina protini kidogo na haina mafuta kama tulivyoona kwa tunda la avocado. Pia ina asili ya wanga, na ni chanzo kizuri cha vitamini B, C na E. Aidha ina madini mengi ikiwemo madini ya chuma. Kuna kitu kinaitwa beta-carotene ambayo imo ndani ya karoti na hii ikiingia mwilini inabadilishwa na kuwa vitamini A. Vile vile karoti ina kirutubisho kinachoitwa fiber ambacho ni muhimu kwa kukinga kuta za utumbo.
Karoti  inasaidia kukinga na kuponya magonjwa kama macho hasa kutoona gizani au kwenye mwanga hafifu, ngozi, kupunguza tindikali inayodhuru tumboni na kukinga magonjwa yenye asili ya kansa.Karoti inaweza kuliwa kwa namna mbalimbali kama vile, ikiwa mbichi kwa kutafuna, inaweza kupikwa na kuchanganywa na mbogamboga zingine, inaweza kusagwa na kupata juisi ambayo pia inaweza kuchanganywa na juisi zingine, aidha kukatwakatwa na kuchanganywa kwenye saladi ya matunda  na mbogamboga. Machicha ya karoti iliyosagwa yanaweza kutumika kama dawa kukinga ama kuponya maradhi ya nje ya mwili. 

                                                       JUISI YA KAROTI
  MAEMBE NI MUHIMU KATIKA KUTENGENEZA SELI ZA DAMU NA KUZILINDA NA BAKTERIA
MACHUNGWA NA JAMII YAKE YANAUWEZO MKUBWA WA KIMARISHA MENO NA MIFUPA 
PARACHICHI LINASAIDIA NGOZI KUWA NA KINGA YA MAGONJWA SHAMBULIZI KUPITIA NGOZI KAMA MBA NA INASAIDIA NYELE KUWA IMARA NA KUREKEBISHA MAFUTA(CHOLESTEROL)


 
KOKOMANGA NI TUNDA LENYE UWEZO MKUBWA KUPAMBANA NA KANSA ZA AINA ZOTE MWILINI.

  NYANYA NI KINGA NZURI YA INI LISIARIBIA AU KUSHAMBULIWA NA BAKTERIA


        NDIZI MBIVU NDIO TUNDA PEKEE DUNIANI LENYE UWEZO WA KUPAMBANA NA VIRUSI VYA UKIMWI 


ZABIBU LINAUWEZO MKUBWA KATIKA KUONGEZA DAMU MWILINI NA KUONGEZA NGUVU WAKATI WA UZEE SIKU ZAKO MAISHA DUNIANI ZIKAONGEZEKA.


                                                     ONYO

  • EPUKA KUNYA JUISI ZA VIWANDANI HAZITENGENEZWI NA MATUNDA HALISI BALI NI KEMIKALI KALI KWA AJILI LA LADHA NA HARUFU YA TUNDA ZINAMADHARA KATIKA MWILI WA BINADAMU KAMA KANSA, INI KUHARIBIKA, DAMU KUWA NA SUMU, ZINAPUNGUZA UMRI WA KUISHI, TAKE CARE JIPENDE KWA KULA NA KUNYA  KILICHO BORA.

RUTO NA KENYATTA WABANWA THE HAGUE

The Hague- Mahakama ya kimataifa imedhidi kuwabana washitakiwa wa makosa ya vurugu  na kusababisha umwajikaji wa damu baaada ya uchaguzi mkuu 2007 nchini Kenya William Rutto na Uhuru kenyatta kwa kutupilia mbali hoja yao ya kuhoji uhalali wa mahakama hio kusikiliza kesi yao. Mahakama hio imepinga hoja yao kwa kusema mashitaka wanayokabiliana nayo ya hadhi kusikilizwa kwenye mahakama hio.
                                   UHURU KENYATTA NA WILLIUM RUTO- THE HAGUE

Thursday, May 24, 2012

MNYIKA ASHINDA KESI

Mbunge wa jimbo la Ubungo John mnyika ameshinda kesi iliyofunguliwa dhidi yake na mpinzani wake Hawa Ng'humbi. kesi hiyo iliyokua ya vuta ni kuvute hatiye jaji wa mahakama hio ametupilia mbali mashitaka yote dhidi ya mbunge huyo.
1)Kwamba Mnyika alimtuhumu kuuza nyumba za UWT
2)Kutumia Laptop za Mnyika Kuhesabu kura
3)Kuingia watu wengi wa CHADEMA katika chumba cha kuhesabia kura
4)Kuzidi kwa kura hewa 16,000
5)Kukosewa kwa karatasi za kujumulisha kura (form). Na mshitaki Bi. Hawa kutakiwa kulipa gharama zote za kesi hio.
        
                    WAFUASI WA CHADEMA HAWAKUWEZA FICHA FURAHA ZAO
            MNYIKA AKIWA NA BI HAWA NG'HUMBI MAHAKAMANI LEO WALIKETI PAMOJA
            MHE; JOHN MNYIKA AKISHANGILIA NA WANACHAMA WA CHADEMA 

MBUNGE WA ROMBO ALALAMIKIA VIJANA

MBUNGE WA JIMBO LA ROMBO JOSEPH SELASINI-CHADEMA ALALAMIKA KUPITIA 

FACEBOOK KWAMBA VIJANA WANAMZUSHIA  KWAMBA HANA USHIRIKIANO NA WANANCHI 

KAMA UNAVYOONA HAPA CHINI. 




Wednesday, May 23, 2012

JE WAJUA! HASIRA/KUSHTUKA KUNA SABABISHA KISUKARI

Utafiti umefanyika nchini marekani umeonyesha kwamba watu wenye hasira na wanoshituka mara kwa mara wako kwenye hatari ya kupata ugonjwa wa kisukari. Kwasababu unaposhtua au ukasirika kongosho huzalisha insulini/glycogen  nyingi haraka zaidi na kuipeleka katika damu  ili kuuapa mwili nguvu kukabiliana na hatari lakini usipofanya kitendo chochote kwa wakati ule wa hasira au mshituko. Tatitizo hujitokea damu inakuwa na sukari nyingi na kusababisha kupata ugonjwa wa kisukari. Unashauriwa unapopata mshituko au hasira fanya kiendo chochote kile cha kutumia nguvu au kimbia umbali fulani kuepuka ugonjwa huo. Pia wanasayansi hawa wamegundua unyaji wa maziwa na vitu vingine vyote vinavyotengenezwa na maziwa mengi vinasababisha kisukari kwasababu maziwa yanasababisha homoni za insulini kuzalishwa zaidi katika mwili. Pia watoto wadogo wanaopewa vyakula vya kwenye makopo/ vilivyotengenezwa viwandani wako hatarini zaidi kupata kisukari na wanawake wanaotumia vidonge vya uzazi wa mpango wanashauriwa watumie kondom zaidi ili kuepuka kisukari


MAZOEZI NI MUHIMU KUEPUKA UGONJWA WA KISUKARI


Tuesday, May 22, 2012

PUTIN ATANGAZA BARAZA LA MAWAZIRI

Rais wa Urusi Vladimir Putin ametangaza baraza la mawaziri la nchi hii. Katika baraza la mawaziri hilo lina mabadiliko madogo katika wizara ya elimu,afya,kilimo, mambo ya ndani, na uchumi. Huko waliobahatika kuendelea kushika nyadhifa zao za mwanzo ni waziri wa ulinzi na mambo ya nje. Putin amemchagua aliyekua mkuu wa polisi nchini humo kuwa waziri wa mambo ya ndani. Putin amejipanga sawasawa kuendeleza uchumi wa Urusi safari hii amemchagua mpinzani wake katika sera za Uchumi kuwa Waziri wa uchumi. Putina ameshindwa kuhudhuria kikao cha G8 kilichofanyika marekani mwishoni mwa wiki iliyopita na kumtuma waziri mkuu amwakilishe pia anakabiliwa na changamoto za ujenzi vituo  vya kuzuia makomboro ulaya ya kati.
         RAIS PUTIN AKIKUTANA NA BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI JIJINI MOSCOW

Monday, May 21, 2012

MMILIKI WA FACEBOOK APATA MKE- MCHINA

Mmiliki wa mtandao wa Facebook Mark Zuckebark ameshangaza wengi alipotoa taarifa ya kwamba ni amemuoa rafiki yake wa siku nyingi anayeitwa Prinscilla Chan. Hivi karibuni Miss Prinscilla alimaliza masomo katika chuo kikuu cha california katia fani ya Udaktari wa watoto. Ni muda mrefu Prinscilla alijulikana kama mpenzi wa millionea Mark Zuckebark lakini si mke wa billionea huyu. Tangazo la mshangao liliwekwa na Mark kwenye Facebook kwamba nimepata mke Prinscilla na kubadili  relatin status yake kutoka single to married with Prinscilla Chan, ujumbe huo kwa muda mchache ulipata like 850000. Kilichoshangaza wengi ni ndoa hii kufanyika kwa siri walialikwa watu 100 tu. na walikua wachumba kwa kipindi cha miaka tisa.
BILLIONEA WA FACEBOOK MARK ZUCKERBERG SIKU YA KIAPO CHA NDOA  WALIVAA HIVI






                  BILIONEA WA FACEBOOK MARK AKIWA NA MKEWE ENZI ZA UCHUMBA
                 WALIKUTANA MARK  ALIPOKUA CHUO CHA HAVARD  2003

Sunday, May 20, 2012

BIG BROTHER 2012 -PREZOO NA DKB NI WAPISHI

Upville 'pacha' DKB na Prezzo walikua wapishi. jikoni kama Prezzo mpishi mkuu walikuja na wazo  la kupika kwa ajili ya mapumziko ya Housemates.
Waliamua kuandaa kuku lakini ilikuwa ni ya wazi kwamba ni vigumu walikuwa hawana elimu juu ya jinsi ya kuiandaa, hii ilikuwa dhahiri wakati   Barbz  msimamizi katika jiko  mara nyingi walimuuliza maswali, je,kuku  anapikwa pamoja na maji? , je,  moto waupikia uwe kiasi gani. lakini 
Barbs hakuweza kuwajibu alikuwa na  haraka kwa kuwafundisha maadili ya jikoni kama msimamizi wa jiko. aliwakumbusha asimguse mwenzako sehemu za miili yao wakati katika jikoni.
                                                           PREZOO NA DKB WAKIWA WANAPIKA 

                                                                  CHIEF COOK PREZOOOO

WAFALME WA ULAYA CHELSEA- 2012

Baada ya mashabiki wengi wa timu mbalimbali za ulaya kuichukulia timu ya chelsea kama moja ya timu mbovu iliyoingia kwenye robo fainali ya UEFA, hatimaye jana kitendawili kimeweza kuteguliwa kwa kuwanyamazisha wote ambao walikua wanaibeza timu hii. Ikumbukwe kwamba hata timu ya taifa ya Zambia ilikua inabezwa hivyo lakini baadae ikafanya maajabu ambapo imejirudia tena kwa Chelsea. Wanaosema ni bahati, waache kwani haiwezi kuwa bahati kuifunga Barcelona na tena ijirudie kwa Beryen. Ni uzoefu na uwezo wa straiker Drogba pamoja na kiungo Mikel Obi ndo umeipa ubingwa wa UEFA. Goli la Drogba la kusawazisha liliweza kuwanyamazisha mashabiki wa timu pinzani na ilitokana na kuweweseka kwa Torres kuingia kitu ambacho kilipunguza mashambulizi ya kina Robben na Ribbery hatimaye dakika 30 kuongezwa bila timu yeyote kuongeza goli. Penalt zilizopigwa na Lampard, Luiz, A.Cole na Drogba ziliweza kuibua nderemo na vifijo uwanjani na kushangaza wengi waliokua wanaibeza timu ya Chelsea.( THE BLUES)
DIDIER DROGBA AKIWA AMINI KAMA ATASTAAFU KWENYE SOKA KWA HESHIMA
                                                                DROGBA AKIMLIWAZA ROBEN-BARYERN MUNICH
                       ABROMOVICH MMILIKI KUSHOTO AKISHANGILIA USHINDI
                    DIDIER DROGBA AKIMTEMBEZA NEUVER KWA PENATI YA USHINDI


WACHEZAJI WA CHELSEA WAKICHEKELEA KOMBE LA KWANZA LA UEFA
  Waziri mkuu David cameroon wa uingereza akishangilia huhu mikono juu goli la ushindi alilofunga Drogba kulia kwake Obama na Germany Chancelor Markel. Pamoja Camerron ni shabiki wa Aston Villa lakini hakusita kuonyesha hisia zake Kwa Chelsea. 
border: 0" />

Translate