Charles Tayler aliyekua rais wa Liberia amehukumiwa na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu kwa ajili ya Sierra Leone leo imetoa adhabu ya kifungo cha miaka 50 jela kwa dikteta wa zamani wa Liberia, Charles Talyor. Akisoma hukumu hiyo muda mchache uliopita, Jaji Richard Lussick amesema kwamba jopo la majaji limeamua kwamba Taylor atatumia kifungo chake kwa awamu moja. Mahakama hiyo ilimtia hatiani Taylor mwenye umri wa miaka 64, hapo mwezi Aprili. Taylor alipatikana na makosa ya kuwafadhili na kuwapa silaha waasi wa United Revolution Front (URF) wa nchi jirani ya Sierra Leone wakati nchi hiyo ikiwa kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe. Katika vita hivyo vya baina ya mwaka 1992 na 2002, kiasi ya watu 120,000 waliuawa. Wakili wa upande wa mashtaka amemPa kifungo cha miaka 80 dhidi ya Taylor. Kesi yake iliyoanza mwaka 2007 ilishuhudia watu kadhaa maarufu wakihusika, akiwamo mwanamitindo wa Kimarekani, Naomi Campbell, ambaye alisimama kizimbani kama shahidi. Kesi hiyo ilihamishiwa kutoka Afrika ya Magharibi na kufanyika nchini Uholanzi kwa sababu za kiusalama
Charles Taylor akiwa The Hague mahakamani
No comments:
Post a Comment