OBAMA ARUHUSU NDOA ZA MASHOGA MAREKANI
Rais wa Marekani Barack Obama anaunga mkono moja kwa moja ndoa za watu wa jinsia moja, akiwa rais wa kwanza kufanya hivyo nchini humo. Obama amesema kuwa alisita, kwa sehemu, kuhusu ndoa za watu wa jinsia moja kwasababu alifikiri kuwa mahusiano ya watu wawili kwa mujibu wa sheria za kiraia yanatosha. Jana katika mahojiano ya televisheni katika ikulu ya Marekani ameeleza kuwa alikuwa na shaka kuhusiana na ukweli kwamba watu wengi neno ndoa ni jambo ambalo linazusha hisia kali za kitamaduni na imani za kidini. Obama amesema kuwa kwa sasa ni muhimu kwake binafsi kujitokeza na kuthibitisha kuwa mahusiano ya watu wa jinsia moja yanafaa kufikia kuwa watu hao wanaweza kuoana.
No comments:
Post a Comment