Watu 55 wafa na 372 wajeruhiwa vibaya.
MAGARI YALITEKETEA NDANI YAKIWA NA WATU.
MILIPUKO HIO IMEACHA MITARO MIKUBWA KAMA UNAVYOONA PICHA YA CHINI.
MILIPUKO HIO IMEACHA MITARO MIKUBWA KAMA UNAVYOONA PICHA YA CHINI.
Syria milipuko miwili mikubwa ambayo imeutikisa mji mkuu wa Syria Damascus a, imefanywa na washambuliaji wa kujitoa muhanga na kusababisha vifo vya watu 55 na watu wengine 372 wamejeruhiwa vibaya. Washambuliaji waliweka zaidi ya kilo 1,000 za milipuko katika magari yao. Hapo kabla vyombo vya habari vya taifa vimesema kuwa milipuko hiyo imewauwa watu 40 na kuwajeruhi wengine 200. Mjumbe wa kimataifa kuhusu Syria Kofi Annan ameshutumu vikali mashambulio hayo katika taarifa iliyotolewa na msemaji wake Ahmed Fawzi. Annan amesema kuwa amesikitishwa na upotevu wa maisha kutokana na mashambulio hayo na anatoa rambi rambi zake kwa familia za wahanga. Annan amesema kuwa vitendo hivi vya kuchukiza havikubaliki na ghasia nchini Syria ni lazima zikome. Nao umoja wa Ulaya umeshutumu vikali mashambulio hayo, na kuyaeleza kuwa ni vitendo vya kigaidi.
No comments:
Post a Comment