Emmanuel Okwi mchezaji wa Simba, Amekua kivutio kikubwa sana. Kwa mashabiki wa soka nchini Sudan. Kwa habari zilizopati toka katika benchi la ufundi la timu ya EL AHLY SHANDY wanahaha jinsi kuwaa walinzi wao mbinu za kumzuia Okwi asiweze kuzifumania nyavu zao.
Mchezo huo ni wamarejeano wa raundi ya 3 ya kombe la shirikisho CAF, na Simba SC wanaitaji sare ya aina yoyote ile ama wasifungwe magoli zaidi ya 2-0 katika mchezo huo. Simba Sport Club waliichapa El Ahly Shandy goli 3-0 katika mchezo uliochezwa april 29 katika uwanja wa Taifa, na kujiweka katika mazingira mazuri ya kutinga katika hatua ya mwisho ya mtoani, ambapo atapangiwa kucheza na moja ya timu zitakazotolewa katika klabu bingwa Africa.
Simba waliwasili Sudan mei 9 usiku bila ya beki wake Said Chollo na Juma Saidi Nyosso kufuatia kutakiwa kukosa mchezo huo, kutokana na adhabu za kadi walizopata. Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa mei 10 na Ofisa Habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga ilieleza kuwa wachezaji wa Simba walitelekezwa hotelini kwa zaidi ya saa tano baada ya wenyeji kuwaambia wangewafuata kwa ajili ya safari ya kwenda mji wa Shendi ambako ndiko mechi hiyo itafanyika. Mechi hio itachezwa jumapili 13 May. saa mbili usiku.
Kikosi hiko baada ya kufika nchini sudan walitekelezwa kwa saa kazaa na baadae waapelekwa kulala mabwenini, chakula wanakipata wa taabu mlo wa mchana wanakula saa kumi jioni. kutokana na hali hio timu ya simba imesema utaifungulia mashitaka timu hio ya sudan kwa shirikisho la soka barani afrika.

No comments:
Post a Comment