Mawakili wapinga Pendekezo la hukumu ya Taylor
Mawakili wa aliyekuwa Rais wa Liberia Charles Taylor wanasema pendekezo la waendesha mashitaka kuwa ahukumiwe kipindi cha miaka 80 gerezani ni cha kulipiza kisasi. Taylor amepatikana na hatia ya makosa 11 ya kusaidia na kuwafadhili waasi katika vita vya Sierra Leone. Mwendesha mashtaka, Brenda Hollis, wiki iliyopita alisema kifungo hicho kirefu kinaweza kuonyesha jukumu kubwa ambalo Talyor alilitekeleza katika uhalifu wa kiwango kikubwa kama hicho. Mahakama hiyo haina adhabu ya kifo. Katika nyaraka zao zilizowasilishwa kabla ya hukumu kutolewa jumatano wiki ijayo, mawakili wa Taylor wamesema adhabu ya maana inapaswa kuwa idadi fulani ya miaka ambayo inapaswa kuwa chini ya kile kinachoweza kuonekana wazi kama kifungo cha maisha gerezani.
No comments:
Post a Comment