Mkutano wa viongozi wa kisiasa na wafanyabiashara wa Kimataifa wameanza mkutano mjini Addis Ababa,Ethiopia kujadili jinsi ya kukuza maendeleo na kuvutia uwekezaji katika bara hilo.
Mkutano huo wa siku tatu juu ya Uchumi Duniani utaangazia masuala kama ajira, utawala bora na kutunza mazingira.
Watayarishi wa mkutano huu wanasema kua Afrika, ni bara lenye nchi sita zenye Uchumi unaokua kwa kasi Duniani na sasa bara hilo liko kwenye ukingo wa mabadiliko makubwa ya uchumi.
Nigeria ni mojapo ya nchi hizo zenye Uchumi unaokua kwa kasi, lakini kama anavyoarifu mwandishi wa BBC Chris Ewokor kutoka Abuja, siyo kila mwananchi aliyenufaika na wimbi hili la mapato.
Ewokor anasema kua majuma matatu yaliyopita Waziri mdogo wa Nigeria katika Wizara ya fedha, Dr Yerima Ngama,alitangaza kua nchi hiyo ni ya tatu kwa nchi zenye Uchumi unaokua kwa haraka.
Alidokezea kua uchumi umeimarika zaidi katika sekta isiyokua ya mafuta, na kwamba serikali ilikua katika jitihada za kuuimarisha zaidi uchumi wake.
Hata hivyo matamshi ya Waziri huyo yanatokea wakati wataalamu wa masuala ya Uchumi nchini Nigeria wakieleza kua nchi hio ina idadi kubwa ya raia wanaoishi maisha duni ya ufukara. Uchumi kwa kiwango kikubwa bado unategemea mafuta. Lakini wa Nigeria wengi ni masikini licha ya utajiri wa mafutla kwa siku
Taarifa ya Benki ya Dunia inasema kua nusu ya watu Afrika wanaishi kwa kipato cha chini ya dola moja kwa kila siku.
No comments:
Post a Comment