Mawaziri wapya wanaoapishwa na Wizara zao kwenye mabano ni Mbunge wa Handeni, Dk Abdallah Kigoda (Viwanda na Biashara), Mbunge wa Kalenga, Dk William Mgimwa (Fedha) na Mbunge wa Kuteuliwa, Profesa Sospeter Muhongo (Nishati na Madini).
Manaibu Mawaziri wapya ni Mbunge wa Rufiji, Dk Seif Suleiman Rashid (Afya na Ustawi wa Jamii), Mbunge wa Kibakwe, George Simbachawene (Nishati na Madini- Nishati), Mbunge wa Bumbuli, January Makamba (Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia), Mbunge wa Buchosa, Dk Charles Tizeba (Uchukuzi) na Mbunge wa Mvomero, Amos Makala (Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo).
Wengine ni Mbunge wa Makete, Dk Binilith Mahenge (Maji), Mbunge wa Shinyanga Mjini, Stephen Maselle (Nishati na Madini ), Mbunge wa Viti Maalumu, Angela Kairuki (Katiba na Sheria) na wabunge wa kuteuliwa, Janet Mbene na Saada Mkuya Salum ambao wote wamekuwa Manaibu Waziri wa Fedha.
Naibu Mawaziri waliopandishwa na kuwa mawaziri kamili ni Christopher Chiza (Kilimo, Chakula na Ushirika), Dk
Harrison Mwakyembe (Uchukuzi), Dk Fenella Mukangala (Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo) na Khamis Kagasheki (Maliasili na Utalii).
Mawaziri wengine waliohamishwa kutoka wizara zao za awali kwenda nyingine ni, Celina Kombani kutoka Katiba na Sheria kwenda Ofisi ya Rais (Manejimenti ya Utumishi wa Umma) ambako amechukua nafasi ya Hawa Ghasia ambaye amehamishiwa Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi).
Shamsi Vuai Nahodha aliyehamia Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa akitokea Mambo ya Ndani, ambako amechukua nafasi ya Dk Hussein Mwinyi ambaye amehamishiwa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.
Dk Emmanuel Nchimbi amehamishiwa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi akitokea Habari, Utamaduni na Michezo wakati Waziri wa Katiba na Sheria sasa ni Mathias Chikawe ambaye alikuwa Ofisi ya Rais (Utawala Bora) na Profesa Jumanne Maghembe amehamishiwa Maji akitokea Kilimo; George Mkuchika ambaye sasa amehamishiwa Ofisi ya Rais – Utawala Bora akitokea Tamisemi na Profesa Mark Mwandosya ambaye ameteuliwa kuwa Waziri katika Ofisi ya Rais, asiyekuwa na Wizara Maalumu. Kabla ya hapo alikuwa Wizara ya Maji.
Manaibu Waziri waliohamishwa wizara zao za zamani zikiwa kwenye mabano ni Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais Charles Kitwanga (Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia), Adam Malima, Kilimo, Chakula na Ushirika (Nishati na Madini) Pereira Ame Silima, Mambo ya Ndani ya Nchi (Fedha).
Wengine ni Gregory Teu, Viwanda na Biashara (Fedha) Lazaro Nyalandu Wizara ya Maliasili na Utalii (Viwanda na Biashara), Jerryson Lwenge Ujenzi (Maji).
No comments:
Post a Comment